Header Ads

ZEE LA NYETI: ...unakomaaje na Bata wakati laifu yenyewe utata?

Jana ilikuwa siku ya mfanano wa kuzaliwa ya mwanangu mwenyewe Mohamed Change, Dj Mzee aliyegoma kukua tauni, anakomaa tu na ishu za naniliu, humu humu tunapigana vkumbo lakini haniwezi, mwenyewe hajui haniwezi kwenye nini, ila anajitahidi kunipiga majungu lakini wapi, …napenya.

Eneweiz mchizi pati yake ilikuwa na mademu kibao mwanangu mwenyewe, kama we mtu wa kumaindi zile ishu ungeibuka, lazima ungeibuka na zigo, gambe zilikuwa za kutosha, watt walipiga kinywaji mpaka wakazima kudadadeki, mwanetu alijipanga.

Umri bwana ukiusherehekea, unapendeza, hata kama sio miaka mia tisa…

Sasa babaako si nikazamia ule mnuso, nikakutana na wazamiaji wenzangu kama nane vivi, walikuwa kwenye meza ya nyuma yangu, mademu flani hivi wenye uspuni tauni, watu wa kusukuma mandinga ya kukodi na pamba kaliiii, za bei ya laki kwenda mbele, ambao ukijimiksi ukakaa nao meza moja unalo. 

Uliza haukamz?

..lazima uachiwe bili hiyo mwanangu, na hawa mademu wanakuwaga fulltaimu wameinama kwenye simu wako bize balaa, na ni bora habari zao za Simu tupotezee maana ukitaka kujua huwa wanaandika nini unaweza ukawachapa vibao kudadadeki.

We si unajifanya jentromeni? Mwenzako anakuona bwege tu..
..ndio bwege, kwani mini babu, unaumia wakati ukweli?
..na kama umemaindi narudia tena unaonekanaga Bwege tu!

Ukiingia tu mezani kwake ukamuuliza kistaarabu kama naweza kukujoini anakukaribisha, halaf anazama wasapu, anawashtua washkaji zake, baada ya muda anaibuka moja moja na vigauni vaya vaya siku hizo kama blauzi.

Mchana wanavivaaga na skintaiti chini, usiku taiti inatupwa, Mzee unafaidi nyama, na mwanangu mwenyewe ninavyokujua lazima uoneshe ujentromeni hapo, watoto wakali tena? zitakuja bili mpaka upagawe, ..si bwege? 

Ujue washkaji tauni hapa wanadhani ujetromeni ni kuvaa fresh, kunukia na kuzama kiwanja, halaf ukiwakuta mademu uwe unapiga raundi. Kumbe mademu wenyewe wana picha tofauti na hão majentromeni, demu wa tauni hataki mambo za kistaarabu sijui Ouganda na mtu, Sao pela pela tu.

Na ndio maana leo ukimuibukia demu sijui umwambie mambo ya ficha yake, umfungulie biznes ya faida kilo kwa wiki anakuona mbwiga tu, kwa sababu mwenyewe akitega tu kiwanja hiyo kilo anaweza kuibabua kwa danga dakika tano tu.

Sasa haukamz umpe mpango wa kumuweka mahala kwa kilo?

Sista dua utamkuta homu ana pamba za Bei mbaya, kiatu kirefu mpaka kule, viwanja anavyopita babu yangu we mwenyewe unajifikiria mara mbili mbili kuibuka, ila sasa kamsachi, ana mkwanja mrefuuuu, sana sana unamkuta na fifte labda, tena wachaaaache.

Huyo sista sasa apate msala labda augue ghafla halaf labda mumrudishe homu, utakoma mwanangu mwenyewe na roho yako, chini utakuta godoro, ndio kitu utakachokielewa labda hivi vingine mpaka uambiwe hiki ni nini.

Haps ndio Zee linachukua apatyuniti na kuongea na masista zeta sasa kuhusu hizi Bata za tauni, mnafkiri zinaisha? Haziishi, miili yenu itazeeka, bata mtaziacha na sisi madanga pia mtatuacha tunadangwa na wanenu. Sasa fainali inafika wakati mnakuwa hamjaweka akiba hata buku, mnabaki kutuachia lawama.

Uso unakuwa ushaweka makunyazi, unafkiri Henry Kibodya atakupigia simu? Lazima akupotezee…
Anakuwa anawapigaia wajukuu zako, ndio anakula nao bata, kwa hiyo shtuka sistaangu, piga Bata huku unajiandalia maisha ya baadae.

Inaitwa laifu afta Bata!

Mama baada ya gambe uwe na pa kulala pasipokuwa na distabansi za Baba mwenye nyumba wala nini, halafu na Akiba uwe nano mwanangu, na Hawa wanaokufadhili kwee kinywaji wape maneno ya maana.

Mtu anakupiga gambe unamwita buzi?

Acha zako sistaangu, eneweiz, mtakuwa mmenielewa kama sio wengi baadhi au sio? Basi tutaonana Jumatatu ijayo, mstue na mshkaji kwamba Zee liso laivu kila Jumatatu lina mwezi sasa, changamkia topiki, na kisha ukishasoma acha komenti


Usisahau lakini ukijifanya jentromeni we bwege tu

No comments

Powered by Blogger.