Header Ads

Wanawake 26 Wanaijeria wafariki baharini Italia

Miili ya wanawake 26, inayoaminika kuwa ya raia wa Nigeria, imepatikana katika ufukwe wa bahari nje kidogo ya pwani ya Italia.

Wanawake hao, ambapo mdogo zaidi kwa umri anaaminika kuwa wa miaka 14, walikuwa wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean kutokea Libya ili kuingia Bara Ulaya.

Haijabainika mara moja kiini kilichosababisha wanawake wengi kiasi hicho kufa kwa wakati mmoja, kwani kulikuwepo pia na wanaume kwenye meli iliyokuwa ikiwasafirisha.

Kuna shaka kuwa, huenda walibakwa na kisha kuuwawa, walipokuwa wakivuka kupitia njia hiyo hatari ya bahari ya Mediterranean.

Waendesha mashtaka nchini Italia, kwa sasa wanachunguza kubaini kiini hasa kilichosababisha maafa hayo, kwani wanawahoji wahamiaji watano katika mji wa bandarini wa Salerno ulioko Kusini mwa Italia.


- BBC Swahili

No comments

Powered by Blogger.