Header Ads

ZEE LA NYETI: Punguza fiksi uishi kama Messi!

Wabongo noma sana, yaani siku hizo ukiwa king’ang’anizi kwenye jambo unaitwa Mugabe, sasa sijui ukiwa mzee wa fiksi utaitwa nani? Maana hawakosi la kusema jamaa, kila siku tunaamka na drama siku hizi, hii nchi hii, ila sihami wala nini, ntazeeka hapa hapa na Paulo ni mshkaji wangu sana, ingawa ni kwa mbaaaali.

Big up kwa mwanangu mwenyewe Dk Shika, tayari shavu limeshamfikia alipo na kaanza kula maisha kiulaini tu, na ninavyowajua wabongo mtaanza na nyie kuleta drama mkiamini mtatumia tobo alilotokea na Dakta Shika na nyie kutusua, msijaribu wanangu, kausheni, kila mtu na andiko lake, Dakta aliandikiwa kutoka mnadani, sasa na nyie mkienda Yono mtaumbuka nawaambia, sio ishu.

Sasa hivi mwanetu unaambiwa Dakta ana mialiko kibao harusini, akikatiza kitaa watu wanamfuata kama Daimondi kipindi anatoka. Sasa sijui kama ataweza kumaintaini iwe ndio ishakubali, kama ilivyokuwa kwa yule mshua wa Loliondo.

Wikiendi ilikuwaje babu?
Ya Kwangju nimeimaliza kwa kula samaki wengi sana bichi kwa hasira, kuna mchizi wangu alinizingua sana wiki hii, sijui mayanki wa kibongo wana akili gani mwanangu mwenyewe. Mpaka leo kuna mchizi anawaza anaweza akatoba kwa fiksi, kweeeli???

Ujue kwenye hizi gambe zeta za kila wikiendi huwa tunakutana na  washkaji wapya, unaona bwana? Sasa pamoja na gambe huwa tunabadilishana Biznes kadi ili baada ya gambe, pengine Jumatatu tukikaa ofisini tunaweza kupeana michongo maisha yakaenda.

Unaona bwana?

Lazima ukae kwa faida kwenye hizi gambe, ishu za kukaa na waganga njaa zishapitwa, tukae chini, tule gambe huku ili zinafanyika, huu ndio mpango.

Sasa bwana, kuna bwana juzi katimba kijiweni kwangu ninakopigaga gambe, akawa kajoini meza yangu, wakati gambe zikiendelea tukamuuliza, mwanetu wewe una mishe gani tauni? Mwanetu akatuchana kwamba yuko kampuni flani ya kutengeneza monde, ya kitambo sana tauni hapa.

Kwa kuwa sana vote pale ni watts wa gambe, tukaona mchizi sio mtu wa kumpoteza, afundi zikaanza kumpitia kwa sana tu, misais na nini…
Kila alipotaka kununua gambe watu tukawa tunamzuia, tunamwambia mwana kausha, wewe mgeni, siku nyingine unanunua.,  Watu walikuwa wanajua jamaa mshua flani ambate miele miele huko atakuja kutufaa.

Basi mwanangu dakika chache, wakaibuka washaji ambao tunawajua wanapiga mzigo kampuni ambayo mwana katuchana, wakaibuka pale wakakaa, stori zikawa zinaendelea.

Sasa tukawa tunashangaa Mona hawakuwa na koneksheni na yule mwana ambaye alituchana kwamba anafanya kazi kampuni hii hii? Ina maana hawajuani au wameamua kuchuniana? 

Sasa bwana kwenye kijliwe si unajua hakukosekani waropokaji? Mmoja akalianzisha bwana, akawauliza wana kama wanamjua mwana, wana wakamkana, mchizi akaanza kutoka jasho pale watu tukamgeukia mwana akawa kama anatetemeka hivi.
..watu tukahama meza….

Mchizi naye akaangalia huku na huku, …akasepa!

Sasa tukaanza kujiuliza kwani fiksi bado imo kwenye fasheni? Halaf inasaidia nini? Maana mwisho wa siku lazima uumbuke, sasa kwa nini mwanangu mwenyewe, unasema uko huku kumbe haupo, sasa hata michongo si itakuwa inakupiga tobo?

Half unalaumu laifu ngumu kumbe fiksi zako ndio zinasababisha mambo yawe sio mambo mwanangu? Potezea fiksi babu, utaishi kama Messi tauni hapa!

Wiki njema wanangu kama vipi wiki ijayo hapa hapa tutakutana
..wanlav…


No comments

Powered by Blogger.