Header Ads

Obama ajitokeza kufanya kazi ya mzee wa baraza Chicago

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama(Pichani juu) alifika katika majengo ya mahakama moja Chicago kuitikia wito wa kuhudumu kama mzee wa baraza la mahakama.

Hata hivyo, jaji alimwamuru aondoke bila kuhudumu.

Umati wa watu ulikusanyika katika jengo la manispaa la Daley Center kumuona rais huyo wa 44 wa Marekani, ambaye ana nyumba katika jiji la Illinois.

Bw Obama aliondoka kwake nyumbani mwendo wa saa tatu unusu saa za huko siku ya Jumatano na aliondoka majengo ya mahakama saa sita hivi mchana.

Kila mtu aliyekabidhiwa wito wa kuhudumu kama mzee wa baraza mahakamani hupokea hundi ya $17.20 (£13.11) kutoka kwa wilaya hiyo.

Helikopta za wanahabari zilitumiwa kupiga picha kutoka juu angani huku msafawa wa Bw Obama wa walinzi wa rais na marais wastaafu maarufu kama Secret Service ukipita kutoka nyumbani kwake mtaa wa Kenwood hadi kwenye jengo hilo la manispaa.

Obama alifika akiwa amevalia jaketi lakini bila tai, kisha ataingia kwenye lifti na kupanda hadi ghorofa ya 17.

Huko, alikutana na wazee wengine wa baraza la mahakama

Baada ya kutazama video ya "kupashwa mengi zaidi kuhusu kazi ya wazee wa baraza la mahakama," Jaji mwandamizi wa wilaya ya Cook Timothy Evans alimwamuru Bw Obama kuondoka.

Baadaye, Bw Obama alitoa hotuba ya kulipwa katika kampuni ya uwekezaji ya GCM Grosvenor, kwa mujibu wa gazeti la Chicago Sun-Times.

-BBC Swahili

No comments

Powered by Blogger.