Header Ads

Cpwaa mbioni kurudi chati za BongoFleva

Msanii Ilunga Khalifa a.k.a Cpwaa ambaye kwa kipindi kirefu takriban miaka miwili na zaidi hajakuwa kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya huenda akarejea jukwaani mwakani, lakini pia kusikika tena kwenye chati za muziki wa kizazi kipya nchini kama ilivyokuwa awali.

CPwaa amethibitisha audio wake katika kipindi cha Uhondo cha Efm alipokuwa akifanya mahojiano kuhusiana na tamasha la nguvu ya kitaa litakalofanyika Jumamosi ijayo, katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam, tamasha ambla litahusisha wasanii wengi wa kizazi kipya wa zamani.

Msanii huyo mwenye asili ya mkoa wa Tanga amesema kwa kipindi chote alichokuwa kimya kimuziki alikuwa akirekodi muziki wake na kuuweka kwenye maktaba zake, huku akitafuta usimamizi mzuri wa muziki wake pindi atakapokuwa tayari kurudi katika medani ya muziki wa kizazi kipya iliyompa umaarufu mkubwa kipindi cha nyuma.

"Nimeshakaa chini na Management maya,


No comments

Powered by Blogger.