Header Ads

ZEE LA NYETI: Ukiona tauni kuna utata, vileji inakuita!


Na Henry Mdimu
Naskia kitaani mlishaanza kuzingua kwa washkaji waliokuwa wakiulizia stori za Zee, naskis mnapakaza mchizi kaishiwa, wengine wanadai kazeeka wengine wanaua kwa kusiliba kwamba mchizi kafulia, hana hata kifaa cha kuandikia, sijui wametoa wapi madishi haya, wakati mtu mzima niliamua tu kuchenji chaneli.

Kwani imekatazwa?

Ila mzuka wanangu, stori zenu zimemtoa nyoka pangoni, mchizi nimeamua kuingia kitaani kuendelea kupiga stori mbili tatu na wanangu kila Jumatatu, kwa staili ile ile lakini safari hii ni Onlaini kama hivi. Najua wanangu wengine ilikuwa ngumu kubebana na mapepa, sasa hivi kitu kiko kwenye smatifoni, unalikamata Zee laivu kudadadeki.

Kwa hiyo wanangu akina Riz Mbwana, Abdi Sultani, Skubi, Hugo naskia mwanangu wamekutupa Wami, watu wabaya mjue? Hivi ukiwa unapiga mzig maeneo ya wham gambe ndio unakula wapi? Hukawii u]kuwa umetulia mahali unakula laga mara Mzee Mamba kaibuka.

Utamweleza nini?
Inakuwa noma na nusu!

Eneweiz bade tupo tauni, na Bata lipo kwa staili ile ile, watu na ishu zetu tauni hapa, tena sio za kitoto, ishu za mamilioni na bado tai huzioni, pamba zile zile za kitaa ta buku mbili jero, tunasonga na wanangu begani kama uji na mgonjwa. Na kimtindo kinaeleweka hatuko juu wala hatuko chini sana, kimsingi tunapambana.

Malalamishi yapo kwa wanetu ambao walikuwa hawajazoea kuchakarika, watu walikuwa wanapiga hela ujue enzi za Jakaya lia sababu ni kwamba mpunga wa mazabe mtaani ulikuwepo. Sasa siku hizi tuna Magu, kaanza kubana zile dili tulizozoea zile, hela imekuwa ngumu haipatikana kizembe kitaa, kila mtu kashtuka anabana mpaka mia, yaani mwanangu ukiokota Buku mtaani nipigie nikuongezee utakuwa kweli una bahati.

Sema nini…

Wanangu sasa mtaani ndio kama wamepata kisingizio cha kuzidi kupiga mizinga watu kama sio kiwakaba kisaikolojia, machizi wanatumia muda mwingi sana kupiga stori za kulalamika kuliko kwenda utafuta vibarua na kupiga kazi.

Huyu Mzee wa kisukuma wanamtaja kweli kitaani kwamba kawabania, lakiniukicheki freshi situesheni, wana wamejibana wenyewe kwa kupenda mteremko. Wengi wa watu wanaopiga stori za kulalamika utakuta ni sana ambao enzi za Jakaya walikuwa ni watu wa kukinga kwa mapedeshee, sasa mapede wenyewe dizaini wamechoka.

Sasa hivi kuliko kumpiga mtu mzinga, ni mpaka uwe na maelezo kamili, pakje kudadadeki, umwambia mkwanja unaompiga mzinga unaenda kuufanya nini, yaani umhakikishie kwamba ukitoka hapo hatakuona tena, tena huyo ni mana mliyeshibana. 

Mwengine hata taimu ya kukusikiliza hakupi…

Na kwa nini uwe watu wa kulalamika wanangu, dili za julima zinalipa, mwanangu mwenyewe Wakuvanga kaona tauni sio ishu katimkia zake Mbwinde sasa hivi analima mipunga huko, Mkandamizaji Iringa na wengine kibao wanapiga dili za Mali shambani. Jakaya mwenyewe anavuna sasa hivi Msoga, wewe nani ung’ang’anie tauni?

Tuwaachie Makonda na Le Mutuz wenye akili kubwa, ndio wanaopaweza

Time babu kama huna ishu, mji waachie wenyewe wenye ishu zao mjini.
..sikutetei wala nini…

Laifu haizingui hata kidogo mwanangu mwenyewe nimekuja kushtuka wewe mwenyewe ndio mzinguaji, unang’ang’ania tauni wakati ishu ya kufanya huna, unaishi kwa taaaabu wakati homu kwenu kuna michongo kibao, halaf unajiita mjanja

Huo sio ujanja mwanangu mwenyewe mimi nakupa laivu. Ukitaka nikuone mjanja unajua upige zipi?

Au ndio nyie wakati ishu ziko poa mlikuwa mmezingua homu hata buku hampeleki? Ndio maana mnaona noma kurudi ama nene?

Sasa mchongo hau happy mwanangu mwenyewe, piga Simu homu, ibuka, mshale ukienda porini haujapotea, unaenda kwao na piga ua lazima utaanguka na mnyama.

Tukutane wiki ijayo mtu mzima nimerudi na nguvu zote, happy ni kila jumatatu Zee litakuwa linasomeka, nawatakia haso njema

No comments

Powered by Blogger.