Header Ads

Waziri Mkuu wa Iceland aelekea kushinda uchaguzi

Waziri Mkuu mhafidhina wa Iceland anatarajiwa kuunda serikali mpya baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu, lakini haijulikana kama atafanikiwa kuunda muungano unaofaa. 

Asilimia 81 ya kura zimeshahesabiwa hadi sasa na hakuna chama kilichoweza kushinda wingi wa kura katika uchaguzi huo wa mapema uliofanyika jana. Huenda ikachukua siku, wiki au miezi kadhaa kabla ya Iceland kupata serikali mpya huku mazungumzo ya kuunda serikali ya muungano yakiendelea. 

Chini ya mfumo wa Iceland, rais humpa mamlaka ya kuunda serikali kiongozi wa chama kilichoshinda wingi wa kura. 

Licha ya kukabiliana na mfululizo wa kashfa za kisiasa, Waziri Mkuu Bjarni Benediktsson na chama chake cha Independence waliibuka kama chama kikubwa katika uchaguzi huo, kwa kunyakua viti 16 katika bunge lenye viti 63.
- DW Swahili

No comments

Powered by Blogger.