Header Ads

UNA HABARI? Rais wa Wakurdi Massoud Barzani ameachia ngazi

Rais wa wakurdi nchini Iraq Massoud Barzani amewacha wadhifa huo wakati eneo hilo linapambana na serikali kufuatia uhuru wake.
Kupitia barua iliyosomwa kwa bunge la Kurdi, Bw. Barzani alisema kuwa hataomba kuongezwa muhula wake ambao unakamilika siku nne zinazokuja.
"Ninaomba bunge kukutana ili kujaza nafasi hiyo," alisema. Wakurdi walikipiga kura mwezi uliopita kuitenga Kurdistan lakini Iraq inasema kuwa kura hiyo ilikuwa kinyume na sheria.
Kisha jeshi la Iraq likaanzisha oparesheni ya kuukomboa mji uliokuwa chini ya wakurdi wa Kirkuk na kuteka vituo vya mafuta vya mji huo. Bwana Barzani alisema atasalia mpiganiaji wa kurdi na atazidi kutetea mafanikio ya watu wa Kurdistan.
Bw Barzani aliingia ofisini mwaka 2005 baada ya kuhusika katika wajibu mkubwa wa kunda eneo huru la Kurdistan lililo kaskazini mwa Iraq baada ya Saddan Hussen kuondolewa madarakani.
Barzani alishinda uchaguzi mwingine wa urais mwaka 2009 na muhula wake ukaongezwa mwaka 2013.
Baada ya kupoteza maeneo yanayozunguka mji wa Kirkuk kwa serikali ya Iraq, alishinikizwa na wapinzani katika eno la Kurdistan kuondoka madarakani.
- BBC Swahili

No comments

Powered by Blogger.