Header Ads

Ujerumani yaadhimisha miaka 500 ya mabadiliko

Viongozi wa kisiasa wa Ujerumani wanakusanyika Jumanne katika mji wa mashariki wa Wittenberg Ujerumani, ili kuadhimisha miaka 500 ya mabadiliko yaliyoanzisha kanisa la Waprotestanti.

Kumbukumbu ya miaka 500 ya mageuzi yaliyofanyika katika kanisa inafanyika leo nchini Ujerumani kwa sala maalum. 

Tarehe 31 Oktoba mwaka 1517 mtawa wa zamani Martin Luther aliweka katika mlango wa kanisa la Wittenberg katika jimbo la Thuringia michanganuo yake maarufu 95. 

Hatua hiyo ni sehemu muhimu hadi hii leo ya vuguvugu la mageuzi duniani kote, ambalo limeligawa kanisa la Katoliki na kuanzisha kanisa la Kilutheri. 

Katika kumbukumbu hiyo katika kanisa la Witternberger watahudhuria pia rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier na kansela Angela Merkel. Kutokana na sherehe za kumbukumbu hiyo, leo ni siku ya mapumziko kwa Ujerumani nzima.

- DW Awahili

No comments

Powered by Blogger.