Header Ads

Tiger Woods kurejea uwanjani karibuni

Mkali wa mchezo wa gofu duniani, Tiger Woods anatarajiwa kurejea tena dimbani katika miezi nane baada ya kuandamwa na majeraha.

Habari zilizoandikwa na tobuti ya BBC Swahili zinasema atajitupa uwanjani kuanzia Novemba 30 mpaka Desemba 3.

Woods mshindi wa vikombe 14 vya kimataifa, anapona majeraha ya upasuaji wa mgongo aliyofanyiwa miaka mitatu iliyopita ambayo kwa wakati fulani alikuwa akirudia upasuaji mara kwa mara na kumfanya kuwa dhaifu.

Alijiondoa katika michuano ya Dubai mwezi Februari kwa sababu hiyohiyo.

''Ninajipanga kurejesha heshima yangu, furaha yangu na uwezo wangu kupitia mchezo ninaoupenda, alisema Woods''

Woods hajashinda taji lolote kubwa tokea mwaka 2008.

No comments

Powered by Blogger.