Header Ads

Mh Mkuchika awasili Ofisini awake Dodoma, awaasa watumishi wenzake kuhusu rushwa na uadilifu

Waziri wa nchi,  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma, na Utawala bora Captent Mstaafu George Mkuchika amewataka watumishi wa ofisi yake kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya utumishi wa umma wakiwa katika kutoa huduma kwa jamii.

Mh Mkuchika ameyasema hayo mara baada ya kuwasili Ofisini wake jijini Dodoma, ambako ndio makao makuu ya nchi. Amewaamba watumishi wa Wizara yake kwamba wanapaswa kuepukana na vitendo haswa vya rushwa wanapokuwa katika kuihudumia jamii.

Ameitaja ofsi take kuwa ndio kioo cha watumishi wote wa umma, na kwamba ndio inayopokea malalamiko mbali mbali ya watumishi kwa hiyo, watumishi wa ofisi yake wanatakiwa kutumia busara ya hali ya juu katika kuhakikisha kwamba wanafanya kazi zao kwa uadilifu.

Pamoja na mambo mengine, Mh Mkuchika ameomba ushirikiano wa hali ya juu na wafanyakazi wenzake.

PICHANI JUU: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika akipokewa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya ofisi yake mjini Dodoma
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika akisalimiana na watumishi wa ofisi yake, mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya ofisi yake mjini Dodoma.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika akizungumza na watumishi wa ofisi yake, mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya ofisi yake mjini Dodoma.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika akisaini kitabu cha wageni ofisini kwake, mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya ofisi yake mjini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akimuonesha moja ya picha za kumbukumbu za makatibu wakuu wa zamani wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika alipomtembelea katibu huyo ofisini kwake, mara baada yairi huyo kuwasili Makao Makuu ya ofisi ya Rais-Utumishi mjini Dodoma.

No comments

Powered by Blogger.