Header Ads

HII HAPA: Story ya Mbunge wa Singida Kaskazini kujiuzulu uanachama wa CCM na nyadhifa nyingine

Na Mwandishi Wetu
Kuna habari zinaendelea kuenea kupitia mitandao na vyombo rasmi via habari susiana na Mbunge wa Singida kaskazini, Mh Lazaro Nyalandu(Pichani juu) kujiuzulu nyadhifa zake za Ubnge m uanachama wa Chama cha Mapinduzi na Ujumbe wa halmashauri kuu ya chama hecho na Mhariri wetu amepokea kauli hiyo ambapo pia inaonekana kwenye akaunti ya Facebook ya Mwanasiasa huyo.

Kauli yenyewe ni nii hapa chini.
Nimeamua rasmi kujiuzuu Nafasi ya ujumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi CCM pamoja na nafasi zote ndani ya chama cha mapinduzi kuanzi aleo Oktoba 30 mwaka 2017

Halikadhalika asubuhi ya leo nimemuandikia Mhe. spika wa Bunge Job Ndugai, barua ya kujiuzulu rasmi nafasi yangu ya ubunge wa jimbo la Singida Kaskazini kupitia CCM, nafasi ambayo nimeitumika kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa mara ya kwanza mwaka 2000 hadi sasa

Aidha nimechukua uamuzi huo kutokana na kutokulidhishwa kwangu na muenendo wa hali ya kisiasa nchini ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa haki za kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa watanzania wenzangu na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi ya mihimili ya dola yaani Serikali, Bunge na Mahakama. Tunapofanya utendaji wa kazi wa kutunga sheria na kusimamia kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana kikatiba.

Vile vile naamini bila Tanzania kupata katiba Mpya sasa hakuna namna yoyote ya kufanya mihimili ya dola isingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali, Bunge na Mahakama ambayo ndio chimbuko na uongozi bora la nchi na kuonyesha kwa wazi kuwa madaraka yote yanatokana na wananchi wenyewe na kwamba serikali ni sharti iwe ya watu kwa ajili ya watt.

Blog mii pia imefanikiwa kupata link ya Youtube ikimuonesha Waziri hiyo wa zamani wa Maliasili na Utalii akithibitisha uamuzi wake

No comments

Powered by Blogger.