Header Ads

Zimbabwe Yatakiwa Kuboresha Miundombinu Ili Kuwavutia Watalii

Tokeo la picha la Zimbabwe National ParkZimbabwe imetakiwa kuboresha miundombinu ya sekta ya utalii na kushusha bei ili kuifanya nchi hiyo iwe na nguvu kubwa zaidi kwenye ushindani katika kusini mwa Afrika.

Ripoti iliyotolewa na Shirika la Habari la Zimbabwe New Ziana na Maoni ya watalii wa Zimbabwe VES, vimeonesha kuwa asilimia 31 ya watu waliofika Zimbabwe waliwatembelea ndugu na marafiki, huku asilimia 29 wakiwa wapita njia, ikifuatwa na watalii halisi wakiwa asilimia 18.

Utafiti huo uliofanywa kati ya mwaka 2015 hadi 2016 na idara ya takwimu ya Zimbabwe kwa niaba ya wizara ya utalii, umependekeza kuwa kuna haja kwa nchi hiyo kutatua suala la gharama kubwa za kutalii nchi hiyo ili kuongeza nguvu ya ushindani.

No comments

Powered by Blogger.