Header Ads

Zidane Ahimiza Umoja Na Mshikamano

Tokeo la picha la real madrid logo
Baada ya kuambulia matokeo ya sare ya mabao matatu kwa matatu, wachezaji wa Real Madrid wameombwa kuendelea kushikamana na kusahau yaliyopita.
Ombi hilo kwa wachezaji wa Real Madrid limetolewa na meneja wao Zinedine Zidane, ambaye alionekana kutoridhishwa na matokeo ya sare ya mabao matatu kwa matatu dhidi ya Las Palmas usiku wa kuamkia leo.
Katika mchezo huo Real Madrid walilazimika kujipanga baada ya kuwa nyuma kwa mabao matatu kwa moja, na walifanikiwa kusawazisha.

Zidane alisema: "Tumepambana na kupata matokeo ya sare kwa pamoja, tunapaswa kuendelea kuwa wamoja, ninaamini tutafanikiwa kumaliza msimu huu tukiwa na kitu mkononi mwetu. Tunapita katika wakati mgumu na tunapaswa kutambua changamoto zinazotukabili sasa, kwani kila mpinzani wetu anakuja kwa kutupania na mwishiwe tunapata wakati mgumu wa kupamabana, lakini hatuna budi kusisitiza umoja kuendelezwa miongoni mwa wachezaji wetu.

No comments

Powered by Blogger.