Header Ads

Zambia Yasaini Makubaliano Na Shirika La GSMA

Tokeo la picha la GSMA Phone

Serikali ya Zambia imesaini makubaliano na Shirika la Mfumo wa Kimataifa wa Mawasiliano ya Simu za Mkononi GSMA ambalo linawakilisha maslahi ya watoa huduma za simu za mkononi, ili kuhimiza usalama wa mtandao wa internet na ulinzi wa watoto kwenye mtandao huo nchini humo.

Kusainiwa kwa makubaliano hayo ni muhimu kwa usalama wa matumizi ya teknolojia ya mawasiliano na habari, ambayo yameweka bayana kwamba watoto wenye umri wa miaka mitano wamekuwa watumiaji wa mtandao wa Internet ambao wanahitaji ulinzi dhidi athari mbaya zinazoweza kuletwa na mtandao huo.

Makubaliano hayo yalisaniwa kando ya Mkutano wa Baraza la Simu za Mkononi Duniani la GMSA unaofanyika huko Hispania.

No comments

Powered by Blogger.