Header Ads

Waziri Maige Ahudhuria Maombi Ya Taifa Yaliyoendeshwa Na Bill Winston Leo Jijini Dar

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MAOMBI kwa ajili ya Taifa yamefanyika leo Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa nA
 
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Agostino Maige pamoja na Mchungaji maarufu na mfanya biashara na mwanzilishi wa Huduma ya Bill Winston, Bill Winston kutoka nchini Marekani.

Mkutano huo uliokuwa na lengo la kuliombea taifa uliweza kuhudhuriwa na viongozi wa dini na serikali na Bishop kutoka nchini Zambia  Bernard Nwaka aliendesha maombi hayo.


Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Agostino Maige akzungumza katika mkutano wa maombi ujulikanao kama Tanzania National Prayer uliofanyika leo Jijini Dar es salaam na kuendeshwa na Mchungaji maarufu na mfanya biashara na mwanzilishi wa Huduma ya Bill Winston, Bill Winston. 

Mchungaji maarufu na mfanya biashara na mwanzilishi wa Huduma ya Bill Winston, Bill Winston akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa maombi kwa taifa ujulikanao kama Tanzania National Prayer uliofanyika leo Jijini.

Aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Dr Oby Ezekwesili akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa maombi kwa taifa ujulikanao kama Tanzania Natipnal Prayer uliofanyika leo Jijini.

Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kingdom Leadeship Network Tanzania (KLNT), Dk. Charles Sokile akijadiliana jambo na Mratibu wa Kamati ya Maandalizi, Carol Mbaga .

Bishop Bernard Nwaka kutoka Zambia akiongoza maombi kwa ajili ya taifa yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Agostino Maige,Mchungaji maarufu na mfanya biashara na mwanzilishi wa Huduma ya Bill Winston, Bill Winston na Aliyewahi kuwa makamu wa raisi wa benki ya Dunia kanda ya Afrika Dr Oby Ezekwesili.

Mkutano ukiwa unaendelea.Picha zote na Zainab Nyamka.

No comments

Powered by Blogger.