Header Ads

Watu 26,000 Wakimbia Mapigano Kutoka Magharibi Mwa Mosul

Tokeo la picha la Jassim Mohammed al-Jaf

Watu 26,000 wamekimbia makazi yao kutoka magharibi mwa mji wa Mosul kutokana na mapambano makali ya kuwatimua wapiganaji wa Kundi la IS kutoka ngome yao kuu ya mwisho nchini Iraq.

Waziri wa uhamiaji wa Iraq Bw Jassim Mohammed al-Jaf amesema wizara yake imewapokea watu hao katika muda wa siku kumi zilizopita kwenye operesheni za kijeshi zilizofanywa magharibi mwa Mosul. 

Vikosi vimewaondoa na kuwahamishia raia hao kwenye kambi zilizoko katika mji wa Qayyara na Hammam al-Alil pamoja na kusini mwa Mosul, na kuwapatia vyakula na dawa.

Mwisho mwa mwezi uliopita waziri mkuu wa Iraq Bw Haider al-Abadi alitangaza kuanza kwa operesheni nyingine ya kuliondoa kundi la IS kutoka magharibi mwa Mosul.

Umoja wa Mataifa umekadiria kuwa watu takriban laki 7.5 hadi 8 bado wanaishi katika maeneo ya magharibi mwa Mosul, idadi ambayo ni changamoto kwa vikosi vya Iraq katika kuingia katika mji huo.

No comments

Powered by Blogger.