Header Ads

Watu 16 Wauawa Katika Mashambulizi Ya Mabomu Mjini Kabul, Afghanistan

Tokeo la picha la afghanistan

Wizara ya afya ya Afghanistan imesema watu wasiopungua 16 wameuawa na wengine 59 wamejeruhiwa katika mashambulizi mawili ya mabomu yaliyotokea mjini Kabul, Afghanistan.

Msemaji wa polisi wa Kabul amesema shambulizi la kwanza lilikuwa ni shambulizi la kujitoa mhanga, lililotokea kwenye lango la makao makuu ya polisi, baada ya polisi kupambana vikali na watu waliojaribu kuingia jengo hilo na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 15 na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa.

Shambulizi la pili lilitokea kwenye makao makuu ya Idara ya usalama ya taifa na kuwajeruhi watu wasiopungua watano. Kundi la Taliban limetangaza kuhusika na mashambulizi hayo.
Rais Ashraf Ghani wa Afghanistan amelaani vikali mashambulizi hayo.

No comments

Powered by Blogger.