Header Ads

Wanawake Wazidi Kumiminika Kufungua Akaunti Ya Malkia CRDB

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Muhamasishaji wa akaunti ya Malkia katika wiki ya wanwake Duniani kutoka benki ya CRDB tawi la Water Front Mary Gekura amesema kuwa mpaka kufikia Machi 06 zaidi ya akaunti 100 za Malkia zimefunguliwa na wakina mama wengi bado wanaendelea kujitokeza kwa wingi.

Mary amesema kuwa kuelekea katika kilele cha Wanawake Duniani bado wanaendelea kuhamasisha wanawake wajitokeze kufungua akaunti hizo kwani zina manufaa kwao na zinawapatia faida baada ya mwaka mmoja.

Akaunti ya Malkia inamuwezesha mwanamke kuweza kupata mtaji au faida ya kujiendeleza kiuchumi baada ya kuifungua na kuweka fedha kwa kipindi cha mwaka mzima bila kutoa.

Muhamasishaji wa akaunti ya Malkia katika wiki ya wanwake Duniani kutoka benki ya CRDB tawi la Water Front Mary Gekura akimkabidhi fomu ya klufungulia akaunti moja ya kina mama waliojitokeza kufungua akaunti hiyo kuelekea kilele cha maadhimisho ya wiki ya wanawake Duniani Machi 08.

 Muhamasishaji wa akaunti ya Malkia katika wiki ya wanwake Duniani kutoka benki ya CRDB tawi la Water Front Mary Gekura akimuelekeza namna ya kujaza fomu  ya kufungua akaunti ya wanawake ijulikanayo kama Malkia.

Wafanyakazi wa CRDB tawi la Water Front wakiwa katika picha za pamoja.

No comments

Powered by Blogger.