Header Ads

Victor Moses Kubaki Stamford Bridge Hadi 2021

Tokeo la picha la Victor Moses

Mshambuliaji kutoka nchini Nigeria Victor Moses amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu ya Chelsea ya England.

Moses amesaini mkataba wa miaka miwili ambao utamuwezesha kukaa Stamford Bridge hadi mwaka 2021.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amekua chachu katika falsafa za meneja Antonio Conte, amekua akitumika mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha The Blues.
"Nimefurahi kukamilisha mpango huu wa kusaini mkataba mpya. Nitakua hapa kwa miaka mingine miwili zaidi, baada ya mkataba wangu wa sasa ambao ulitarajiwa kufikia kikomo mwaka 2019," Alisema Moses.


"Tuna msimu mzuri, na kila mmoja anafurahia matokeo tunayoyapata, ninawaahidi mashabiki na wachezaji wenzangu, nitaendelea kuwa mpambanaji hadi tutakapofanikisha azma ya kutwaa ubingwa wa England mwishoni mwa msimu huu."

No comments

Powered by Blogger.