Header Ads

Uvumi Wa Max Allegri Kuhamia Emirates Stadium Waendelea Kushika Kasi

Tokeo la picha la Max Allegri to Arsenal - sky sports

Meneja wa mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC Max Allegri ameendelea kuhusishwa na taarifa za kumrithi Arsene Wenger huko kaskazini mwa jijini London.

Mtandao wa Calciomercato umeripoti, Allegri amefichua siri kwa kuwaambia rafiki zake wa karibu kuhusu uwezekano wa kupewa ajira ya kukinoa kikosi cha Arsenal mwishoni mwa msimu huu, ambapo mkataba wa Wenger utafikia kikomo.

Mtandao huo umeeleza kuwa, Allegri amewaambia rafiki zake suala la kutaka kutwaa ubingwa wa nchini Italia ili aondoke mjini Turin kwa heshima.

Aliwaambia tayari mambo yote ya kuelekea kaskazini mwa jijini London yalipo makao makuu ya klabu ya Arsenal yamekaa vizuri, na kwa sasa anamalizia jukumu la kukiongoza kikosi cha kibibi kizee kuelekea kwenye ubingwa ili asitishe mkataba wake.

Allegri mwenye umri wa miaka 49, mara kadhaa amekua akikanusha taarifa za kuhusishwa na mpango wa kumrithi Arsene Wenger kwa kusema bado yupo yupo sana huko Juventus Stadium.

Huenda taarifa zilizochapishwa kwenye mtandao wa Calciomercato zikaibua mambo mapya kuhusu mustakabali wa kocha huyo kutoka nchini Italia, kutokana na ukimya wa viongozi wa klabu ya Juventus uliotawala kwa kipindi kirefu.

No comments

Powered by Blogger.