Header Ads

UNAIDS Yaanzisha Kampeni Ya Kuondoa Ubaguzi Dhidi Ya Wagonjwa Wa Ukimwi

Tokeo la picha la UNAIDS

Shirika la kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa UNAIDS limeanzisha kampeni ya kuondoa ubaguzi dhidi ya wagonjwa wa Ukimwi, likiwataka watu kutoa sauti za kupinga vitendo au kauli za kibaguzi. 

Takwimu kutoka nchi 50 zinaonesha kuwa mmoja kati ya watu wanane wanaoishi na virusi vya HIV hukataliwa huduma za matibabu, na karibu asilimia 60 ya nchi za Ulaya zimeripoti kuwa unyanyapaa na ubaguzi miongoni mwa wafanyakazi wa afya umekuwa kizuizi dhidi ya utoaji huduma za kuzuia maambukizi ya virusi vya HIV kwa wanaume wanaofanya ngono ya jinsi moja na watu wanaojidunga dawa za kulevya.

No comments

Powered by Blogger.