Header Ads

UN Waitaka Korea Kaskazini Isimamishe Majaribio Ya Makombora

Naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Fahan Haq amesema katibu mkuu Bw. António Guterres ameilaani Korea Kaskazini kwa kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu kinyume cha maazimio ya Baraza la usalama la umoja huo, na kuitaka nchi hiyo isimamishe majaribio hayo na kutekeleza wajibu wake wa kimataifa.

Kamati ya wanadhimu wa jeshi la Korea Kusini jana ilisema Korea Kaskazini ilirusha makombora manne kwenye bahari ya mashariki mwa Peninsula ya Korea, mara ya pili baada ya nchi hiyo kufanikiwa kurusha kombora mwezi uliopita.

Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vimesema Rais wa Korea kaskazini Bw. Kim Jong-un alisimamia majaribio hayo na amelipongeza jeshi lake kwa kazi nzuri.

No comments

Powered by Blogger.