Header Ads

Umoja Wa Nchi Za Kiarabu: Mapema Kujadili Suala La Kuirudisha Syria Kwenye Umoja Huo


Katibu mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu Bw. Ahmed Abul-Gheit amesema ni mapema sana kujadili suala la kuirudisha Syria kwenye Umoja huo.

Akizungumza baada ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Umoja huo, Bw. Gheit amesema, Umoja huo unapaswa kuwa na uvumilivu na kufanya uamuzi baada ya kusikiliza maoni ya pande mbalimbali.

Katika mkutano huo, waziri wa mambo ya nje wa Iraq Bw. Ibrahim Jarari alisema, Syria haiwezi kutengwa na Umoja wa Nchi za Kiarabu, na kwamba nchi za kiarabu haziwezi kuipuuza Syria, hivyo ni lazima kurudisha Syria kwenye Umoja wa Nchi za Kiarabu.

No comments

Powered by Blogger.