Header Ads

Umoja Wa Mataifa Wahimiza Pande Zinazopambana Yemen Kuwaachia Huru Askari Watoto

Tokeo la picha la Ravina Shamdasani

Ofisi ya kamishna mwandamizi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya haki za binadamu OHCHR imezihimiza pande zinazopambana nchini Yemen kuwaachia huru askari watoto, na kusema idadi ya askari wototo nchini humo sasa inakaribia 1,500 tangu mwezi Machi mwaka 2015.

Msemaji wa ofisi hiyo Bi Ravina Shamdasani amesema kuna ripoti nyingi kuhusu utumikishaji wa watoto jeshini nchini Yemen.

Ameongeza kuwa kuanzia tarehe 26 Machi mwaka 2015 hadi tarehe 31 Januari mwaka huu, Umoja wa Mataifa umethibitisha idadi ya watoto waliosajiliwa kuwa askari imefikia 1,476, wote wakiwa ni wavulana.

Bi Shamdasani ameonya kwamba idadi halisi ya askari watoto huenda ni kubwa zaidi, kwa kuwa familia nyingi hazithubutu kuripoti usajili wa watoto wao kwa kuhofia kulipizwa kisasi. 

Bi Shamdasani amezionya pande zote kwamba utumikishaji wa watoto jeshini unakiuka sheria za kimataifa.

No comments

Powered by Blogger.