Header Ads

Umoja Wa Afrika Waahidi Kushirikiana Na Waziri Mkuu Mpya Wa Somalia

Tokeo la picha la Hassan Ali Khaire

Mwakilishi maalumu wa katibu mkuu wa tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM Bw. Francisco Madeira amesema atashirikiana kwa karibu na waziri mkuu mpya wa Somalia Bw. Hassan Ali Khaire ili kutuliza hali ya nchi hiyo.

Bw. Madeira amesema ana imani na Bw. Khaire ambaye aliapishwa kuwa waziri mkuu na kuahidi kuimarisha usalama na kupambana na ufisadi. Ameongeza uzoefu wa Bw. Khaire katika kazi za kibinadamu na biashara utakuwa muhimu kwa serikali mpya.

Habari kutoka tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo UNSOM zinasema, Somalia imefungua kituo cha kurekebisha tabia kwa wapiganaji wa zamani wa kundi la Al-Shabaab katika mji wa Kismayu.

Kituo hicho ambacho ni cha nne kuzinduliwa nchini humo ni sehemu ya Mradi wa Taifa wa Somalia unaolenga kuwapokea na kuwarekebisha wapiganaji wanaojitoa kutoka kwenye mapigano.

No comments

Powered by Blogger.