Header Ads

Ujerumani Yashuhudia Matukio 3,500 Ya Uhalifu Dhidi Ya Wahamiaji Mwaka 2016

Tokeo la picha la germany flag

Wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani imesema mwaka jana nchi hiyo ilishuhudia matukio 3,500 ya uhalifu dhidi ya wahamiaji, idadi ambayo inapaswa kuchukuliwa tahadhari. 

Kwa mujibu wa wizara hiyo, matukio hayo yalihusisha watuhumiwa zaidi ya 2,300, na kusababisha watu 560 kujeruhiwa, wakiwemo watoto 43. 

Wizara hiyo imesisitiza kuwa serikali ya Ujerumani inachukua hatua kali kukabiliana na vitendo hivyo vya uhalifu, na kutoa wito kwa jamii kushiriki katika kupambana na ubaguzi wa kikabila na siasa kali.

No comments

Powered by Blogger.