Header Ads

Uingereza Yakubali Yaishe, Kumaliza Tofauti Zake Na Urisi

Tokeo la picha la 2018 fifa world cup

Kamati ya bunge la Uingereza imetoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kutumia fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 zitakazofanyika nchini Urusi, kurekebisha uhusiano mbaya baina ya Uingereza na Moscow, uliodumu tangu vita baridi.

Kamati ya mambo ya Nje ilionyesha wasiwasi wake endapo Urusi inastahili kuwa mwenyeji wa fainali hizo kutokana na rekodi mbaya iliyonayo kuhusiana na haki za binaadamu.


Ingawa kamati hiyo iliongeza kusema kwamba, badala ya Uingereza kugomea fainali hizo, serikali inapaswa kutumia mwanya wa mashindano hayo kuboresha uhusiano wa mataifa hayo mawili, kwa kuongeza wafanyakazi wa kidiplomasia pamoja na ushirikiano wa polisi kujiandaa kwa lolote litakalojiri kwenye umati wa watu.

No comments

Powered by Blogger.