Header Ads

Ubora Wa Hewa Nchini China Waendelea Kuboreshwa


Waziri wa mazingira wa China Bw. Chen Jining amesema tangu China ianze kuteleleza mpango wa kusimamisha uchafuzi wa hewa, ubora wa hewa ya China umeinuliwa kwa ufanisi.

Bw Chen amesema hayo jana alipokutana na waandishi wa habari kando ya mkutano wa tano wa bunge la 12 la umma la China. Amesisitiza kuwa, mwaka huu wizara yake itaendelea kuimarisha nguvu ya utekelezaji wa sheria, na kutovumilia vitendo vya ukiukaji wa sheria ya uchafuzi wa mazingira. 

Bw. Chen Jining amesema, "Tutaendelea na operesheni ya kutekeleza sheria ya hifadhi ya mazingira, kutilia mkazo usimamizi wa kiutawala sawa na ukaguzi wa viwanda, kuadhibu vikali vitendo vya uhalifu sawa na kusimamia kwa makini utekelezaji wa sheria. 

Pia tunatakiwa kuboresha utungaji wa sheria husika, kuendelea kuongeza nguvu ya utekelezaji wa sheria, kukagua na kutosamehe vitendo vya uhalifu wa kuchafua mazingira, ili kutekeleza kihalisi sheria ya hifadhi ya mazingira. "

No comments

Powered by Blogger.