Header Ads

Trump Alitaka Bunge Kupitisha Mpango Wa Uwekezaji Wa Miundombinu


Rais Donald Trump wa Marekani amesema atalitaka bunge kupitisha mpango wa kuwekeza dola za kimarekani trilioni 1 kwenye miundombinu nchini Marekani ili kutoa mamilioni ya nafasi za ajira.

Rais Trump amesema, mpango huo wa uwekezaji utafadhiliwa kupitia mitaji ya serikali na sekta binafsi, na utaongozwa na kanuni mbili muhimu ambazo ni "Nunua Marekani, na ajiri Mmarekani" ambayo itazinufaisha kampuni za ujenzi, uhandisi, na usanifu za Marekani na wafanyakazi wa Marekani.

Kuhusu mageuzi ya kodi, rais Trump amesema timu yake ya kiuchumi inaandaa mageuzi ya kihistoria ya kodi ambayo yatakata kiwango cha kodi kwa makampuni na wakati huohuo, kutoa nafuu kubwa ya kodi kwa tabaka la kati.

No comments

Powered by Blogger.