Header Ads

Taharuki Yatanda Afrika Kusini Kufuatia Wenyeji Kuwashambulia Wageni

Tokeo la picha la south african flag

Msemaji wa Polisi wa jimbo la Gauteng nchini Afrika Kusini Kanali Lungelo Dlamini, amesema watu watano walikamatwa Jumatatu usiku huko Johannesburg kwa kuvamia maduka na kufanya vurugu.

Polisi wa Afrika Kusini waliwasindikiza wageni nje ya mji wa Jeppestown baada ya kutishiwa Jumatatu usiku. 

Polisi hao walilazimika kuingilia kati baada ya wakazi wenye chuki dhidi ya wageni kuanza kupora maduka ya wageni kwenye eneo hilo, polisi walilazimika kutumia maguruneti na risasi za mpira.

Kanali Dlamini amesema polisi wamewaonya wananchi wanaofanya uhalifu huo kuwa vitendo vyao havitavumiliwa.

Aidha amewataka watu kuripoti matukio ya vitisho, vurugu na uporaji kwenye vituo vya polisi vya karibu.

No comments

Powered by Blogger.