Header Ads

Sudan Yasikitishwa Na Zuio Jipya La Wahamiaji La Marekani

Picha inayohusiana

Rais Donald Trump wa Marekani amesaini amri mpya inayozuia raia wa nchi sita ikiwemo Sudan kuingia Marekani ndani ya siku 90. Serikali ya Sudan imeeleza kusikitishwa na kitendo hicho cha Marekani.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Sudan amesema Iraq imeondolewa kwenye zuio hilo, lakini Sudan bado ipo. Ameitaka Marekani izingatie kazi muhimu zinazofanywa na Sudan katika kupambana na ugaidi na kuiondoa Sudan kwenye orodha ya nchi zinazounga mkono ugaidi.

Waziri wa mambo ya uchumi wa nchi hiyo Bw. Badr-Eddin Mahmoud Abbas amesema kutokana na vikwazo vya Marekani vilivyowekwa tangu mwaka 1997, nchi hiyo imepoteza dola takriban bilioni 45 na kushindwa kulipa madeni ya nje.

Baadhi ya maofisa wa Marekani walisema lengo la zuio hilo ni kulinda usalama wa taifa na raia wake, na itaanza kutekelezwa tarehe 16 mwezi huu.

No comments

Powered by Blogger.