Header Ads

Somalia Yatoa Wito Wa Kuhakikisha Usambazaji Wa Misaada Ya Kibinadamu

Tokeo la picha la rais Farmajo wa Somalia
Mashirika 44 ya misaada yanayofanya kazi nchini Somalia yametoa wito wa kuondoa vikwazo kwenye usafirishaji wa misaada ya kibinadamu kwa ajili ya waathirika wa ukame wanaokumbwa na njaa.

Wito huo umetolewa kwenye mkutano ulioitishwa na rais Farmajo wa Somalia huko Mogadishu, na kuitaka serikali isimamishe kwa muda masharti mapya kwa mashirika ya misaada, ili yaweze kukabiliana na ukame huo unaowaathiri watu zaidi ya milioni 6.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano inasema washiriki wamekubaliana kuchukua hatua za dharura ili kuzuia maafa mengine ya njaa yasitokee, na kuvuruga mafanikio yaliyopatikana katika miaka 5 iliyopita.

Wawakilishi wa mashirika hayo pia wamemwandikia barua katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw Antonio Guterres kumtaka aihimize jumuiya ya kimataifa kuongeza juhudi, na kuepuka makosa ya mwaka 2011.

No comments

Powered by Blogger.