Header Ads

Ronald Koeman Aendelea kumuota Wayne Rooney

Ndoto za meneja wa klabu ya Everton Ronald Koeman za kutaka kumuona mshambuliaji Wayne Rooney akirejea Goodison Park zimeendelea kutawala kichwani mwake.

Koeman amerudia na kuweka msisitizo wa kutamani kufanya kazi na mshambuliaji huyo wa klabu ya Man Utd, alipohojiwa kwenye kipindi cha Sky Sports News HQ.

Rooney mwenye umri wa miaka 31, aliondoka Everton akiwa na umri wa miaka 18, na kwa sasa amekuwa na mazingira magumu ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Man Utd.
Koeman mara kadhaa amewahi kuzungumza katika mikutano na waandishi wa habari kuhusu mpango wa kutaka kumsajili Rooney, na alijaribu kufanya hivyo mwezi Januari mwaka huu, lakini ilishindikana.
Tokeo la picha la Ronald Koeman - sky sports
Hata hivyo meneja huyo kutoka nchini Uholanzi, amesema juhudi zake za kuushinikiza uongozi wa The Toffees ili jambo hilo lifanikiwe zinaendelea hasa katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa msimu huu.
"Wayne Rooney ni mchezaji wa kiwango cha juu na alifanya maamuzi sahihi ya kujiunga na Man Utd akiwa na umri mdogo," said Koeman.
"Bado ana uwezo wa kucheza katika kiwango cha juu kwa miaka mingine miwili ama mitatu ijayo, na ningependa amalizie soka lake Goodison Park ambapo bado mashabiki wanamkumbuka kwa kazi nzuri aliyoifanya akiwa Everton kabla ya kuondoka mwaka 2004.
"Ni mara chache kuwa na wachezaji mwenye kiwango kama cha Rooney ambao hutaka kumaliza soka lake pale alipoanzia, na kwangu mimi ninaamini jambo hilo litatokea kutokana na mazingira yanayomkabili hivi sasa huko Old Trafford."

Rooney alitajwa kuwa katika harakati za kuhamia nchini China, lakini kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili hapo jana huko mashariki ya mbali, mshambuliaji huyo alikanusha taarifa hizo na kusisitiza anataka kubaki Old Trafford.

No comments

Powered by Blogger.