Header Ads

Romelu Lukaku: Nataka Kuipa Mataji Everton FC

Tokeo la picha la Romelu Lukaku - sky sports
Mshambuliaji Romelu Lukaku amesema bado ni mwenye furaha ya kuendelea kuitumikia klabu ya Everton inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini England, japo inakabiliwa na changamoto ya ukame wa mataji.
Lukaku, alijiunga moja kwa moja na Everton akitokea Chelsea mwaka 2013 baada ya kusajiliwa kwa mkopo wa mwaka mmoja ambapo alionyesha uwezo mkubwa na kuwashurutisha viongozi wa The Toffees kumsajili kwa ada ya uhamisho ya Pauni milioni 28.
Mshambuliaji huyo kutoka nchini Ubelgiji, amezungumzia msimamo wa kufurahishwa na maisha ya Goodson Park, baada ya kuulizwa mustakabali wake klabuni hapo, kufuatia mkataba wake kutarajia kufikia kikomo mwaka 2019 katika kipindi cha Sky Sports News HQ.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, ameserma dhamira yake ni kutaka kuisaidia Everton kutwaa mataji na kutamba kwenye michuano ya kimataifa kama ligi ya mabingwa barani Ulaya na Europa League.

Amesema ni mapema mno kuzungumzia mustakabali wake, japo anatambua miaka miwili ijayo mkataba utafikia kikomo, ila amesisitiza suala la kuendelea kukipiga klabuni hapo kwa moyo wote.

"Ni kweli ninataka kuona tunafikia malengo ya kutwaa ubingwa wa England ili tuwe sehemu ya watakaotajwa kama mabingwa wa ligi kubwa ka PL.
"Kama unataka kuwa mchezaji mkubwa ni lazima ufikie malengo uliojiwekea, kwangu mimi nimedhamiria kucheza hapa ili nifanikishe suala la kuipa ubingwa Everton ambayo ninaipenda na kuithamini.
“Utaona kwa wachezaji wengine kama Messi, Ronaldo, Thierry Henry – wote hawa wamefanikiwa baada ya kujituma wakati wote, nataka iwe hivyo na kwangu pia.” Alisema Lukaku.
Lukaku amekua tegemeo kubwa katika safu ya ushambuliaji ya Everton na mwishoni mwa juma hili, anatarajiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji kwenye mchezo wa ligi kuu ya England dhidi ya  Tottenham Hospurs.

Mpaka sasa mshambuliaji huyo ameshaifungia Everton mabao 45 katika michezo 95 aliyocheza.

No comments

Powered by Blogger.