Header Ads

Robo Fainali Azam Sports Federation Cup


Michezo miwili ya kwanza ya hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Azam (Azam Sports Sports Federation Cup 2016/2017), itachezwa Machi 18, mwaka huu kwenye viwanja viwili tofauti.

Michezo hiyo ni  kati ya Kagera Sugar itakayocheza na Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani Kagera kadhalika Simba itakayosafiri hadi Arusha kucheza na Madini kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Michezo mingine itapangiwa tarehe za baadaye. Michezo hiyo  ni kati ya Azam FC na Ndanda FC kadhalika Tanzania Prisons ya Mbeya itakayocheza na mshindi kati ya Young Africans ya Dar es Salaam na Kiluvya United ya Pwani.

Bingwa wa michuano hiyo kwa mujibu wa kanuni, atazawadiwa Tsh. 50 milioni. Pia bingwa wa michuano hiyo, ndiye atakayeiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ya Total wakati Bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ndiye ataiwakilisha nchi kwenye michuano ya Total Ligi ya Mabingwa Afrika.

No comments

Powered by Blogger.