Header Ads

Real Madrid Watakiwa Kujipanga Kwa De Gea

Tokeo la picha la De Gea

Bosi wa kikosi cha Man Utd Jose Mourinho amechimba mkwara wa haja kwa kuwatumia salamu viongozi wa mabingwa wa soka barani Ulaya Real Madrid, kwa kuwaambia mlinda mlango David de Gea atawagharimu kiasi kikubwa cha pesa.

Mourinho amechimba mkwara huo huku akitaja jina la Rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez, ambaye ameonyesha kuwa mstari wa mbele kuhakikisha mlinda mlango huyo anatua Stantiago Berbnabeu wakati wa usajili wa majira ya kiangazi.

Mourinho aliwaambia waandihi wa habari kuwa, Real Madrid wanapaswa kujipanga kuhusu usajili wa mlinda mlango huyo, na kama watakaa hovyo, huenda wasimpate kirahisi kama wanavyofikiia.

Alisema mlinda mlango huyo ana thamani kubwa na ikitokea Man Utd inaridhika na kiasi cha pesa watakacho kitangaza kama ada yake ya usajili, hatokua na hiyana kumruhusu De Gea kuondoka.

Mwanzoni mwa msimu wa 2015/16, De Gea alikaribia kuondoka Man Utd baada ya kuhusishwa kwa kipindi kirefu na taarifa za kurejea mjini Madrid, lakini dakika za mwisho uongozi wa Real Madrid ulishindwa kufikia lengo hilo.


Wakati huo Man Utd walikua tayari kumuuza De Gea kwa kiasi cha Euro milioni 70.

No comments

Powered by Blogger.