Header Ads

Real Madrid Waendelea Kutetea Taji La Ulaya

Tokeo la picha la ssc napoli 1-3 real madrid 07-march-2017

Beki na nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos aliisaidia klabu hiyo kupata ushindi wa mabao matatu kwa moja katika mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya SSC Napoli usiku wa kuamkia leo.

Real Madrid walitanguliwa kufungwa bao la mapema na wenyeji wao katika dakika ya 24 kupitia kwa Dries Mertens.

Kipindi cha pili dakika ya 51 Real Madrid walisawazisha kwa bao lililofungwa na Sergio Ramos kabla ya Dries Mertens hajajifunga mwenyewe dakika sita baadae.

Alvaro Morata alifunga bao la tatu na la ushindi kwa Real Madrid dakika ya 90, na kuhitimisha safari ya SSC Napoli ya kuusaka ubingwa wa barani Ulaya msimu huu wa 2016/17.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza ambao ulichezwa mjini Madrid, Real Madrid walichomoza na ushindi wa mabao matatu kwa moja, hivyo wamesonga mbele kwa jumla ya mabao sita kwa mawili.

Michuano hiyo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya inaendelea tena leo kwa michezo mingine miwili ambapo.

Barcelona Vs Paris Saint Germain

Borussia Dortmund Vs Benfica

No comments

Powered by Blogger.