Header Ads

Rais Wa Sudan Awasamehe Waasi 259 Wa Kundi La Upinzani

Tokeo la picha la Omar Al-Bashir

Rais Omar Al-Bashir wa Sudan amesaini amri ya kuwasamehe waasi 259 wa kundi la upinzani waliohukumiwa adhabu ya kifo.

Waliosamehewa ni pamoja na waasi waliokamatwa na jeshi la serikali huko Darfur, na wengine wengi ni wapiganaji wa kundi la upinzani SPLM tawi la kaskazini, waliokamatwa katika majimbo ya Blue Nile na na Kordofan Kusini.

Habari zinasema kitendo hicho ni kujibu hatua ya kundi la SPLM kuwaachia huru askari zaidi ya 100 wa jeshi la serikali.

Mwezi Septemba mwaka jana, rais Al-Bashir alitangaza kuwa atawasamehe wafuasi wa makundi ya upinzani kama watakubali kuweka chini silaha zao. Pia ameahidi kuwaachia huru askari watoto wa makundi ya upinzani.

No comments

Powered by Blogger.