Header Ads

Rais Wa Korea Kusini Aondolewa Madarakani

Tokeo la picha la Park Geun-hye

Rais Park Geun-hye wa Korea Kaskazini amevuliwa wadhifa wake kama rais wa nchi hiyo baada ya mahakama ya katiba kupitisha hoja ya kumwondoa madarakani.

Kaimu Jaji mkuu Lee Jung-mi amesoma hukumu hiyo kuhusu kumwondoa rais Park madarakani, akisema uamuzi huo ni umefikiwa kwa pamoja na mahakimu wanane.

Wananchi wa Korea Kusini waliokuwa nje ya mahakama hiyo ambao walitaka rais huyo ajiuzulu, walishangilia wakati hukumu hiyo ilipokuwa ikitangazwa moja kwa moja kwa njia ya televisheni.

Uchaguzi wa rais nchini humo utafanyika baada ya miezi miwili.

No comments

Powered by Blogger.