Header Ads

Pogba Chupuchupu Kupigwa Na Mashabiki

Image may contain: one or more people and outdoor
Mchezaji wa Manchester United, Paul Pogba nusura achapwe na mashabiki wa timu hiyo kufuatia kile mashabiki hao walichokiita ukosefu wa adabu na kujivuna kulikopitiza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Polisi wa jiji la Manchester, Pogba akiwa katika matembezi yake ya jioni aliingia katika mgahawa uliopo Liverpool Road jijini humo ambapo aliwakuta mashabiki wa Manchester United waliofika hapo kwa chakula cha jioni waliompokea kwa furaha na nderemo.
Kama ilivyo kwa mashabiki wa soka wanapokutana na wachezaji wanaowashabikia, walimwomba Pogba awasainie vitabu vyao vya kumbukumbu maarufu kama ‘autograph’. Hata hivyo, katika hali isiyotegemewa na wengi, Pogba aliwakatalia.
Hapo ndipo ilipozuka vurugu huku washabiki hao wakitoa maneno ya kashfa dhidi yake na wengine kutaka kumnasa vibao ambapo walinzi wa mgahawa walifanya kila jitihada ili kumwokoa wakati wakiwaita Polisi. Vurugu hiyo iliongezeka na kusababisha Pogba kurushiwa sahani yenye chakula.
Polisi walifika eneo hilo na kukuta mashabiki wenye hasira wakiwa wametawanyika. Baada ya Polisi kufika, Pogba alitolewa na kuruhusiwa kuondoka kwani hali ilikuwa imetulia.

No comments

Powered by Blogger.