Header Ads

Pambano La Amir Khan Na Manny Pacquiao Lafutwa

Tokeo la picha la Amir Khan Vs Manny Pacquiao

Promota Bob Arum wa pambano wa bondia wa Uingereza Amir Khan na bingwa wa uzani wa Welterweight Manny Pacquiao ametoa taarifa za kulifuta pambano hilo pasi na kutoa sababu za kina.

Pambano la wababe hao wawili lilitangazwa kufanyika Aprili 28 mwaka huu, kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter mwishoni wa mwezi Februari, na lilipangwa kufanyikia huko Falme za kiarabu UAE.

Arum alitangaza kulifuta pambano hilo kupitia kituo cha televisheni cha ESPN cha nchini Marekani.

''Ninazungumzia kuhusu pendekezo jingine lakini sio Khan. Khan hatakuwa mpinzani wa Manny''.

Pambano hilo la mwezi Aprili lilipangwa baada ya mashabiki wa Paqcuiao katika mtandao wa Twitter kumpigia kura Amir Khan kuwa mpinzani ambaye wangependelea bondia huyo mwenye umri wa miaka 38 kupigana nae.


Khan mwenye umri wa miaka 30 aliyeshinda medali ya fedha katika uzani wa Lightweight kwenye michuano ya Olimpiki mwaka 2004, alimshinda Kell Brook, raia wa Australia Jeff Horn na Mmarekani Terence Crawford kwa asilimia 48 ya kura hizo zilizopigwa na mashabiki wa Pacquiao.

No comments

Powered by Blogger.