Header Ads

Max Allegri Akanusha Taarifa Za Arsenal Kwa Mara Ya Tatu

Tokeo la picha la Max Allegri - sky sports
Meneja wa mabingwa wa soka nchini Italia Juventus Max Allegri amekanusha kwa mara nyingine kuhusu kufanya mazungumzo na viongozi wa Arsenal, kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Arsene Wenger mwishoni mwa msimu huu.
Allegri amekanusha taarifa hizo baada ya kuulizwa kwa mara nyingine na waandishi wa habari nchini Italia, baada ya mchezo wa ligi ya Sirie A ambapo Juventus walibanwa Udinese na kuambulia matokeo ya sare ya bao moja kwa moja.
Meneja huyo alisema hajafanya mazungumzo na yoyote, na anaendelea kushangaa kuendelea kuhusishwa na mpango wa kutaka kujiunga na Arsenal.
Alisema taarifa hizo kila siku zimekua zikipikwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini Italia kwa makusudi ya kutaka kumpotezea lengo la kufanya vizuri akiwa na Juventus msimu huu.
“Tetesi hizo zinatokea wapi? Maana uongozi wa Juventus ulipaswa kujua kwanza kabla yenu waandishi, sasa inakuaje nyinyi mnaniuliza suala hili ambalo kwanza ninalizisia kwenu? Alihoji meneja huyo.
 “Kama suala hilo lipo tutazungumza na wahusika, na kama halipo mtaona wenyewe, sio kuzusha mambo wakati hayapo. Mpaka sasa sijazungumza na yoyote.”
Allegri mwenye umri wa miaka 49, hajawahi kusema kama ataachana na Juventus FC mwishoni mwa msimu huu, zaidi ya vyombo vya habari kuendelea kuibua tetesi za kuondoka kwake mwishoni mwa msimu huu.
Mkataba wake na klabu ya Juventus bado una muda wa miaka mitatu na utafikia kikomo mwaka 2020.

Kuhusishwa kwake kuelekea kaskazini mwa jiji la London yalipo makao makuu ya klabu ya Arsenal, kunatokana na meneja Arsene Wenger kutarajia kuondoka mwishoni mwa msimu huu, kufuatia mkataba wake kufikia kikomo.

No comments

Powered by Blogger.