Header Ads

Mauro Icardi: Sijutii Kuondoka FC Barcelona

Tokeo la picha la Mauro Icardi, - sky sports

Mshambuliaji wa Inter Milan Mauro Icardi, amesema hajawahi kujutia maamuzi ya kuachana na FC Barcelona ambayo ilitumia muda mwingi kumkuza na kumuendeleza kisoka.

Mshambuliaji huyo tegemeo katika kikosi cha Inter Milan, alikuzwa na kuendelezwa kwenye kituo cha vijana cha FC Barcelona kiitwacho La Masia, kabla ya kufanya maamuzi ya kutimkia nchini Italia mwaka 2011 na kujiunga kikosi cha vijana cha Sampdoria.

Icardi ameliambia gazeti la Marca la Hispania kuwa, maisha ya soka yanastawi popote, na anaamini bado safari yake ya soka inaendelea na huenda kuna siku akajikuta akirudi FC Barcelona kama itabidi.

Amesema anaamini kuna baadhi ya rafiki na watu wake wa karibu wanahisi anajutia maamuzi aliyoyachukua ya kuondoka FC Barcelona yanamuumiza, lakini jambo hilo kwake sio tatizo kutokana na kutimiza hitaji la kucheza soka kama alivyotarajia tangu akiwa na umri mdogo.

"Nilifanya uamuzi mzuri na katu sitojutia, kwa sababu nilitambua kuja kwangu Italia kutaweza kunipa nafasi ya kucheza soka la ushindani,” Alisema mshambuliaji huyo raia wa Argentina.

“Huwezi kujua, huenda ningeendelea kukaa FC Barcelona nisingweza kupata nafasi ya kucheza kama ilivyo hapa Italia, maana ninapata nafasi ya kucheza kila mwishoni mwa juma tena katika kikosi cha kwanza, kwa hiyo ninafurahia maisha ya hapa.” Aliongeza Icardi.

Klabu ya Inter Milan ilimsajili Icardi mwaka 2013 akitokea Sampdoria kwa ada ya Euro milioni 6.5.


Mpaka sasa Icardi ameshaitumikia Inter Milan katika michezo 116 na kufunga mabao 64.

No comments

Powered by Blogger.