Header Ads

Makosa Ya Askofu Mokiwa Yaanikwa Hadharani

Tokeo la picha la Askofu MokiwaWaraka wa Askofu Mkuu wa Anglikana nchini, Jacob Chimeledya umesomwa katika makanisa yote ya Dayosisi ya Dar es Salaam ukibainisha makosa yaliyofanywa na Askofu Valentino Mokiwa na kumtaka kujiuzulu wadhifa wake.
 
Waraka huo umesomwa katika Kanisa la Mtakatifu Albano na mjumbe wa Halmashauri ya walei wa Dayosisi hiyo, Helen Mkoma ambapo Waraka huo umebainisha kuwa Januari 28 mwaka huu, Askofu Chimeledya aliunda kamati ya kwenda kuzungumza na Askofu Mokiwa wakimtaka ajiuzulu kwa hiari ili kulinusuru kanisa hilo.
 
Hata hivyo, Askofu Mokiwa aliomba muda wa wiki mbili ili kutafakari suala hilo lakini wiki mbili zimekwisha hajatoa mrejesho wowote huku kukiwa na viashiria vya kwamba hayuko tayari kutii agizo hilo

No comments

Powered by Blogger.