Header Ads

Lacazette Kuziba Nafasi Ya Daniel Sturridge

Tokeo la picha la Alexandre Lacazette Feb 2017
Klabu ya Liverpool itajaribu kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa Alexandre Lacazette mwishoni mwa msimu huu.
Gazeti la The Daily Mirror limechapisha taarifa hiyo na kueleza kuwa, mshambuliaji huyo wa klabu ya Olympique Lyon anafikiriwa kutua Anfield kufuatia mkanganyiko ulioibuka kuhusu mustakabali wa Daniel Sturridge.
Jurgen Klopp anaamini Lacazette atatosha kukidhi haja ya kuongeza nguvu katika safu yake ya ushambuliaji kwa msimu ujao, baada ya kuona mapungufu msimu huu.
Uongozi wa Olympique Lyon umeshatangaza thamani ya Lacazette ambayo inafikia Pauni milioni 60, na alikua akiwindwa na klabu ya Arsenal mwanzoni mwa msimu huu, lakini uhamisho wake ulishindikana.

Kwa msimu huu Lacazette, tayari ameshaifungia Olympique Lyon mabao 22 katika michezo 23 aliyocheza.

No comments

Powered by Blogger.