Header Ads

LA GALAXY Kumpeleka Marekani Zlatan Ibrahimovic

Tokeo la picha la Zlatan Ibrahimovic to LA Galaxy
Klabu ya LA GALAXY huenda akaharibu mipango ya Man Utd ya kutaka kumbakisha mshambuliaji wao kutoka nchini Sweden Zlatan Ibrahimovic, kwa kumsainisha mkataba mpya kabla ya mwisho wa msimu huu.
LA GALAXY inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Marekani imeonyesha dhamira ya kumsajili Zlatan mwishoni mwa msimu huu, huku ikiweka dhamira ya kumlipa mshahara mkubwa kuliko wachezaji wote wanaocheza katika ligi hiyo.
Kwa mujibu wa Tovuti na Sports IllustratedLA GALAXY wapo makini na jambo hilo na wanaamini wana uwezo wa kumshawishi mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 35, hadi akakubali kujiunga nao mwishoni mwa msimu.
Man Utd wamewahi kuthibitisha kuwa kwenye mazungumzo na Zlatan kwa ajili ya kumsainisha mkataba mpya, lakini muhusika alipohojiwa na vyombo vya habari alisema suala la kusaini ama kutosaini litafahamika mwishoni mwa msimu huu.

Zlatan alisaini mkataba wa mwaka mmoja alipojiunga na Man Utd mwanzoni mwa msimu huu akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Ufaransa PSG, baada ya kuwa huru.

No comments

Powered by Blogger.