Header Ads

Kombe La FA: Kivumbi Kutimka Leo, Man City Kuisaka Robo Fainali Kwa Huddersfield

Manchester City leo usiku watakuwa na kibarua cha kuisaka robo fainali ya raundi ya 5 ya FA Cup ambapo watakutana na Huddersfield Town huko Etihad Stadium.

Mshindi wa Mechi hii atatinga Raundi ya 6 ambayo ndio Robo Fainali na kucheza Ugenini na Middlesbrough.

Mechi za robo fainali za raundi ya 6 ya kombe hilo, zitachezwa kuanzia Machi 11 na moja ya mvuto mkubwa ni Mabingwa Watetezi Manchester United kutua Stamford Bridge kupambana na Vinara wa EPL, Ligi Kuu England, Chelsea.

Arsenal wao watakuwa Nyumbani Emirates kucheza na Lincoln City, Timu ambayo haipo Mfumo rasmi wa Ligi huko England, ambayo ilijizolea sifa kubwa kwa kuibwaga Burnley wanaocheza EPL na waliokuwa Nyumbani kwao.

No comments

Powered by Blogger.