Header Ads

Kikao Cha Kamati Ya Utendaji TFF

Kikao cha kawaida cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la soka nchini TFF , kinatarajiwa kukaa Machi 26, mwaka huu ambako pamoja na ajenda nyingine, itaamua tarehe rasmi ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu.

Kikao hiki cha kawaida, kwa mujibu wa katiba hufanyika mara nne kwa mwaka na huamua masuala mbalimbali ya uendeshaji na usimamizi wa mpira wa miguu nchini.

Kadhalika Mkutano Mkuu wa uchaguzi kwa mujibu wa Katiba ya TFF, hufanyika kila baada ya miaka minne kwa mwaka.

No comments

Powered by Blogger.