Header Ads

Kenya Yazindua Mfumo Wa Kielektroniki Wa Kufuatilia Usafirishaji Wa Mizigo

Tokeo la picha la John Njiraini - kenya

Kenya imezindua mfumo wa kielektroniki wa kufuatilia usafirishaji wa mizigo ili kusimamia kwa wakati wote mizigo inayopitia Kenya wakati iko ndani ya mipaka yake.

Kamishna mkuu wa Mamlaka ya Kodi ya Kenya KRA Bw. John Njiraini amesema, Kenya inajiunga na Uganda na Rwanda ambazo tayari zinatumia mfumo huo.

Mfumo huo mpya ni hatua muhimu ya kuimarisha ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kuhimiza biashara ya kuvuka mipaka.

Mfumo huo mpya utachukua nafasi ya mfumo uliopo wa ECTS, ambao usimamizi wa mizigo unafanywa kupitia majukwaa tofauti.

No comments

Powered by Blogger.